Tuesday, October 23, 2012

REDDS MISS TANZANIA KUPATA SH. MILIONI 8 NA GARI... WA MWISHO KUONDOKA NA SH. 700,000

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza zawadi za mshindi wa shindano la Redds Miss Tanzania 2012. Kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza zawadi za mshindi wa shindano la Redds Miss Tanzania 2012. Kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro.
Meneja wa Kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza zawadi ya mshindi wa taji la Redds Miss Tanzania 2012. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga.

Meneja wa Kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza zawadi ya mshindi wa taji la Redds Miss Tanzania 2012.MSHINDI wa taji la urembo la Redd's Miss Tanzania 2012 ataondoka na Sh. milioni 8 pamoja na gari, waandaaji kampuni ya Lino Agency wametangaza leo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, mkurugenzi wa kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga alisema warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania watachuana katika fainali za shindano hilo litakalofanyika Novemba 3, 2012 kwenye ukumbi wa Blue Pearl Hotel (Ubungo Plaza) jijini Dar es Salaam.

Alisema mshindi wa pili atapata zawadi ya pesa taslimu Sh. milioni 6.2, wa tatu Sh. milioni 4, wa nne Sh. milioni 3, wa tano Sh. milioni  2.4 na kwamba mshindi wa sita hadi wa 15 kila mmoja atapata Sh. milioni 1.2.

Aliongeza kuwa washiriki wengine wote waliobaki yaani wa 16-30 kila mmoja apata Sh. 700,000.

Alisema katika shindano hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo, tayari washiriki watatu wameshajipatia tiketi ya kuingia katika Top 15, ambao ni Lucy Stephano aliyeshinda taji la Miss Photogenic, Magdalena Roy aliyetwaa taji la Top Model na Mary Chizi (Top Sport Woman).

Lundenga alisema shindano dogo jingine la kumtafuta mrembo wenye kipaji, Miss Talent, lifanyika Ijumaa Oktoba 26, 2012.

Aliongeza kuwa mshindi wa shindano dogo la Miss Personality atapatikana Oktoba 28, 2012.

Naye meneja wa kinywaji cha Redds Original, Victoria Kimaro amesema huu ni wakati mwafaka wa kumpata mshindi bomba mwenye vigezo sahihi na hivyo akawataka wapenzi wote wa fani ya urembo na wapenda maendeleo kote nchini kujiandaa kupata tiketi za kushuhudia fainali hiyo mapema ili kupata fursa ya kupata burudani mbalimbali.

"Kwa kweli tunatarajia shindano la mwaka huu litafana sana hasa kwa kuzingatia kuwa maandalizi yote yameshakamilika kwa kiwango kikubwa. Na sisi kama wadhamini wakuu tunahakikisha kuwa mwaka huu kila atakayefika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza atakuwa na jambo la kusimulia kwa sababu ni shindano la kipekee," alisema Vicky.

Shindano la Redds Miss Tanzania 2012 linadhaminiwa na
Kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Original, Star TV na Giraffe Hotel

Mshindi wa mwaka jana alikuwa ni Salha Israel, ambaye alizawadiwa gari aina ya Jeep Patriot lenye thamani ya Sh. milioni 72 pamoja na fedha taslimu Sh. milioni 8.

No comments:

Post a Comment