Wednesday, October 3, 2012

RAMOS: SIKUVAA JEZI YA OZIL KUMPINGA MOURINHO

Sergio Ramos

BEKI wa Real Madrid, Sergio Ramos amekanusha madai kwamba alihoji utawala wa kocha Jose Mourinho wikiendi. 


Ramos alicheza kipindi cha pili cha mechi yao dhidi ya Deportivo La Coruna akiwa amevaa jezi ya Mesut Ozil ndani ya jesi yake - baada ya Mjerumani huyo kutolewa na Mourinho wakati wa mapumziko. 

Gazeti la Marca lilibebwa na habari kuu iliyosema 'Ramos ampinga Mou' wakiambatanisha na picha inayomuonyesha Ramos akiwa na jezi ambayo ndani yake inaonyesha kuna jezi nyingine yenye jina la Ozil.

Lakini Ramos ameandika kwenye Twitter: "Mesut ni rafiki yangu na nilishasema tangu zamani kwamba goli langu la kwanza msimu huu litakuwa ni kwa ajili yake na nilivaa jezi yake nikitegemea kufunga. Hakuna cha zaidi."

No comments:

Post a Comment