Wednesday, October 3, 2012

PUYOL NJE YA KIKOSI BARCELONA KWA MIEZI MWILI


Carles Puyol akipata huduma ya kwanza kabla ya kutolewa nje ya uwanja kwa machela baada ya kuteguyka kiwiko cha mkono katika mechi yao ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Benfica mjini Lisbon jana.  (Picha: Reuters)
MADRID, Hispania
JERAHA la kuteguka kiwiko cha mkono litamuweka Carles Puyol nje ya uwanja kwa takriban miezi miwili na hiyo inamaanisha kuwa kocha Tito Vilanova wa Barcelona atakabiliwa na tatizo jingine la ulinzi wa kati katika mechi yao ya 'Clasico' kwenye La Liga, Ligi Kuu ya Hispanai dhidi ya Real Madrid Jumapili.

Katika mechi yake ya kwanza tangu apone jeraha la goti, Puyol alianguka vibaya kipindi cha pili katika ushindi wao wa 2-0 wa mechi ya Kundi G la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Benfica na klabu yake imesema kuwa atakuwa nje kwa takriban wiki nane.

No comments:

Post a Comment