Wednesday, October 3, 2012

MOURINHO: MAHUSIANO YANGU NA MKE WANGU NI MAZURI KULIKO NA RAMOS

Jose Mourinho

KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amesisitiza hana matatizo na Sergio Ramos.

Kulikuwa na madai jana kwamba Ramos alikuwa akiomba kuondoka Real kutokana na mahusiano mbaya na Mourinho.

Lakini kocha huyo amesema: "Mahusiano yangu na mke wangu ni mazuri kuliko na Sergio Ramos, lakini mahusiano yangu na yeye ni bora kuliko yalivyo na watu nisiofanya kazi nao na ambao sishirikiani nao kila siku.

"Iko hivyo pia katika mahusiano yangu na Arbeloa na wengine. Kuhusu alichokisema kamuulizeni mwenyewe."


Sergio Ramos anadaiwa kuvutana na Mourinho na anasemekana alivaa jezi ya Ozil ndani ya jezi yake na akawa akicheza mbele kwa muda mrefu kusaka goli ili akifunga ashangilie kwa kuvua jezi yake ya juu ili ionekane ya ndani ya Ozil katika kuonyesha sapoti yake kwa kiungo huyo Mjerumani ambaye amekuwa akiwekwa benchi na Mourinho.

No comments:

Post a Comment