Friday, October 12, 2012

PODOLSKI APOTEZA NAMBA TIMU YA TAIFA, ASEMA YUKO TAYARI HATA KUCHEZA BEKI WA KUSHOTO

Lukas Podolski

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Lukas Podolski amedai kwamba atakuwa tayari kucheza hata kama atapangwa kama beki wa kushoto katika timu yake ya taifa ya Ujerumani baada ya kupoteza namba yake katika kikosi cha kwanza cha kocha Joachim Low. 

Katika mechi mbili zilizopita za kampeni ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Jamhuri ya Ireland na Sweden Podolski alicheza kwa dakika 15 tu katika kila mechi. 

"Kila mtu anahitaji kucheza, lakini la muhimu ni kutimiza malengo yetu makuu. Haijalishi nafasi gani nitachezeshwa. Hata beki wa kushoto nitacheza!"

No comments:

Post a Comment