Friday, October 12, 2012

'PARK JI-SUNG KAFUATA PESA TU QPR'

Kocha wa Queens Park Ranger, Mark Hughes (kushoto) na kiungo wa Korea Kusini, Park Ji-Sung siku walipotangaza kusajiliwa kwa nyota huyo kutoka Manchester United kwa ada ya uhamisho ambayo haitajwi katika mkutano na wanahabari mjini London Julai 9, 2012. Park alijiunga na QPR akitokea Man United kwa mkataba wa miaka miwili. Picha: REUTERS
Park Ji-Sung akiwa mzigoni QPR
Park Ji-Sung akiwa mzigoni QPR
Park Ji-Sung akiwa mzigoni QPR


SHUJAA wa Manchester United, Park Ji-sung ameshutumiwa kwa uhamisho wake wa kutua katika timu ya QPR ambayo haijashinda mechi hata moja hadi sasa ikihaha mkiani mwa Ligi Kuu ya England. 

Kiungo wa zamani wa QPR, Lee Cook, amesema: "Kila mara nilipomuangalia Park akiwa Man U, alikuwa akifanya kazi kama punda. 

"Kwa mtazamo wangu hivi sasa hajitumi kama alivyokuwa kule. Najua baadhi ya watu wako pale kufuata pesa tu. Nusu ya msimu ikifika, mtaweza kuona kama haya ninayosema ni kweli au siyo."

No comments:

Post a Comment