Friday, October 12, 2012

'JEMBE' INIESTA LAACHWA NJE MECHI YA HISPANIA v BELARUS LEO ILI AJE AWASHUKIE UFARANSA JUMANNE

Iniesta

WAKATI wa mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi ya kuwanmia kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 mjini Minsk, kocha Vicente Del Bosque alibainisha kwamba Andres Iniesta hataanza katika kikosi cha kwanza cha mechi yao ya leo usiku dhidi ya Belarus, kwa sababu kocha anataka kumpumzisha kiungo huyo wa Barca kwa ajili ya mechi ngumu dhidi ya Hispania Jumanne.

"Tunaifikiria mechi dhidi ya Ufaransa na suala la Andres ni 'spesho'. Nina hakika angeweza kucheza mechi zote mbili, lakini tunahitaji kumlinda kidogo kwa sababu ndio amerejea kutoka kuwa majeruhi wa misuli," alisema kocha huyo.

"Tunao wachezaji kwenye kikosi ambao wanaweza kucheza vizuri katika nafasi yake," alisema Del Bosque. "Mabadiliko sio tatizo. tunafahamu kwamba itakuwa ni vyema kwake asipocheza kwa dakika 180, lakini tutacheza mechi zote hata kama mambo hayataenda sawa. Ni ishu 'sposho'," aliongeza.

Majeraha ya misuli aliyokuwa akiyazungumzia Del Bosque yalimuweka Iniesta nje ya uwanja katika mechi kadhaa na yalianzia katika mechi nyingine ya mchujo ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Georgia.

No comments:

Post a Comment