Friday, October 12, 2012

LYON WALIPEWA 'BURE' CRISTIANO RONALDO WAKAMKATAA

Ronaldo akishangilia goli lake

OLYMPIQUE Lyon ingeweza kumsajili nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kwa bei sawa na bure, imebainika. 

Kocha wa wakati huo wa Sporting Lisbon, Laszlo Boloni alitaka kumsajili Tony Vairelles kutoka Lyon kwa kubadilishana na wachezaji wawili akiwamo Ronaldo. 

"Sporting de Portugal hawakuwa na pesa hivyo walipendekeza kubadilishana wachezaji na walikuwa tayari kuwatoa wachezaji wawili, mmoja wao akiwa ni Cristiano Ronaldo, lakini Olympique walikataa ...," alibainisha Boloni. 

Muda mfupi baadaye Ronaldo akasajiliwa na Manchester United na yaliyobaki yakawa historia.

No comments:

Post a Comment