Saturday, October 6, 2012

MOURINHO: NINA FURAHA TELE REAL MADRID ... SIONDOKI HADI NIMALIZE MKATABA MWINGINE NILIOSAINI WA MIAKA MINNE ... BAADA YA HAPO NAWEZA KURUDI ENGLAND..!

Mourinho

Mzee wa Mataji... Mourinho
MADRID, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho amesema kuwa ana furaha tele katika klabu yake inayoshikilia ubingwa wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania na kwamba hafikirii kuondoka kabla ya kumalizia mkataba mwingine mpya aliosaini hivi karibuni wa kubaki klabuni hapo kwa miaka minne zaidi.

Mourinho ametoa ufafanuzi huo kufuatia uvumi uliotanda kwamba yuko mbioni kurudi kufundisha katika klabu za Ligi Kuu ya England.

“Nina furaha na ninataka kubaki hapa. Nimesaini mkataba mwingine na Real Madrid utakaonibakiza kwa miaka mingine minne, ni kwa sababu sisi ni klabu bora zaidi duniani.

“Kufuatia mataji niliyotwaa England na Italia, Real Madrid ilikuwa inakosekana katika CV yangu. Na sasa kwa sababu tayari ninayo, ninapaswa kufanya kazi kwa uwezo wangu wote.

“Hata hivyo nilikuwa na furaha sana jijini London, na nitarudi tu.”

No comments:

Post a Comment