Ronaldo na Messi |
Hata ukinuna tuzo ya FIFA Ballon d'Or yangu tu...! Messi na Ronaldo wakisalimiana. |
Kocha Jose Mourinho wa Real Madrid (kushoto) akipeana mkono na kocha Tito Vilanova wa Barcelona. |
Straika Leo Messi amefanya mahojiano na todobarcelona.net kuhusiana na masuala mbalimbali ya klabu yake ya Barcelona.
Katika mahojiano hayo, straika huyo wa kimataifa wa Argentina aliulizwa pia kuhusiana na kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho na kusema: "José Mourinho ni kocha mzuri na tena anayeijua vyema kazi yake".
Alipochokozwa kwa swali kuhusu Cristiano Ronaldo, Messi alieza vilevile kwamba straika huyo wa Real Madrid "ni mchezaji mkali".
Nyota huyo wa Barca alisema anaamini kuwa "mchezaji kiongozi ni yule anayeheshimiwa na kila mmoja kikosini... kwa sababu ya namna alivyo na pia kwa sababu huzungumza na wachezaji wenzake pale inapobidi".
Kuna mengi yanazungumzwa kuhusiana na ujio wa Neymar kwenye kikosi cha Barcelona na, kuhusiana na hili, Messi hakutaka kubashiri.
"Kuja kwa Neymar ni jambo ambalo litategemea uamuzi wa benchi la ufundi."
Alipoulizwa kuhusu ushindi wa Tito Vilanova katika mechi chache alizoongoza tangu awe kocha wa Barcelona, Messi alisema kuwa wakiwa naye (Vilanova);"tutaiona Barcelona ileile tuliyoiona katika misimu iliyopita. Tuna namna yetu ya kucheza ambayo haiwezi kubadilika kwa sababu fikra za Tito ni kama Guardiola".
Messi alisisitiza kwamba katika soka huamini katika "kusahau mambo mabaya wanayosema watu, kwa sababu kila kitu hubishaniwa katika mchezo huu".
No comments:
Post a Comment