Saturday, October 13, 2012

MOURINHO: ITAKUWA KASHFA KAMA RONALDO HATASHINDA TUZO YA BALLON D'OR

Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo

KOCHA Jose Mourinho amefanya mahojiano na Bola TV ambapo amemminia sifa Cristiano Ronaldo ambazo hajawahi kumpa, huku akisema CR7 anapaswa kushinda tuzo ya Ballon d'Or ya Mwanasoka Bora wa Dunia.

"Itakuwa ni kashfa kama hatashinda," Mourinho alisema.

Mourinho pia alifafanua sababu za kuwabwatukia wachezaji wake baada ya kumalizika kwa mechi ya 'Clasico', ambapo alidai kuwa "kuwalinganisha nani zaidi baina ya Messi na Cristiano kupigwe marufuku. Messi na Cristiano ni wa nje ya dunia hii."

Mourinho alisema: "Jumapili, baada ya mechi nzuri, niliulizwa nichague na nilijaribu kuja na jibu la haki na heshima kwa wachezaji wote, sio kwa mchezaji wangu tu bali na wa wapinzani pia. Lakini baadaye nikafikiria, mtu mwingine katika nafasi yangu anaposema mchezaji wake yuko nje ya dunia hii, watasema: Wangu hakuzaliwa Madeira, ametokea kwenye sayari ya Mars na, na kwa maana hiyo, si wa duniani. Hivyo ni bora wa ulimwengu."

Sifa alizompa Cristiano Ronaldo hazikuishia hapo na akasema si sahihi kuwalinganisha Messi na Ronaldo: "Na nikasema. Ni vigumu kuwa Ronaldo kuliko Messi. Messi amekulia katika timu na wachezaji wenzake kikosini. Cristiano amekuja hapa akitokea England, kwenye timu ambayo imeyumba. Alilazimika kukua ndani ya miaka miwili katika timu ambayo ndiyo kwanza inakua."

No comments:

Post a Comment