Tuesday, October 9, 2012
MISS MBULU AWA WA KWANZA KUINGIA 16-BORA REDDS MISS TANZANIA 2012
Na Mwandishi Wetu, Monduli
LUCY Stephano ambaye ni Redds Miss Mbulu jana usiku alikuwa mshiriki wa kwanza kuingia katika hatua ya 16-Bora ya Redd’s Miss Tanzania 2012 baada ya kutwaa taji la Redds Miss Photogenic katika shindano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Emanyata Lodge, uliopo mjini hapa.
Lucy aliwashinda warembo wengine 30 wanaoshiriki Redds Miss Tanzania na kufanikiwa kutwaa taji hilo.
Mrembo huyo alitwaa taji hilo baada ya ushindani mkali uliokuwepo kati yake na Redds Miss Dar Indian Ocean, Diana Hussein na Redds Miss Ilala namba mbili, Magdalena Roy.
Kutokana na kutwaa taji hilo, Lucy amepiga hatua moja kubwa zaidi kuelekea taji la Redds Miss Tanzania 2012 linalotarajiwa kufanyika Novemba 3, mwaka huu.
Mrembo mwingine anayetarajiwa kuingia hatua hiyo atapatikana Jumamosi katika ‘Usiku wa Redd’s Miss Tanzania’ mjini Arusha pale vimwana watakapochuana katika kinyang’ayiro cha Miss Top Model.
Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment