Tuesday, October 9, 2012

J-LO KUMBE SHABIKI WA REAL MADRID

Jennifer Lopez akiwa ametinga jezi ya klabu anayoishabikia ya Real Madrid akiwa pamoja na watoto wake mapacha

WAKATI wa ziara ya hivi karibuni kwa ajili ya kuimba katika tamasha la mjini Madrid, Jennifer Lopez alitumia muda wake kupozi akiwa na jezi za Real Madrid pamoja na watoto wake mapacha.

Muimbaji huyo alitumbuiza kwa wimbo wa 'Palacio de los Deportes' baada ya mechi ya 'Clasico'.

"Nakupenda Madrid! Asante kwa upendo mlionionyesha", aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

Katika soka pia, Lady Gaga hivi karibuni alibainisha kwamba yeye ni shabiki wa Barcelona wakati akitumbuiza stejini.

Mwanadada Shakira hivi sasa ana ujauzito wa beki wa Barcelona, Gerard Pique.

 

No comments:

Post a Comment