Sasa hivi natisha kinoma...! Jack Wilshere wa Arsenal akiwatoka Shaun Wrights Phillip na Esteban Granero wa QPR wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates leo, Oktoba 27, 2012. |
Wilsherer wa Arsenal (kulia) akifanya vitu vyake leo, Oktoba 27, 2012 |
Kashakash langoni mwa Wigan wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya West Ham United leo, Oktoba 27, 2012. |
Niache huko...! Hapa ni mshikemshike katika mechi ya Ligi Kuu ya England kati ya Stoke na Sunderland leo, Oktoba 27, 2012. |
LONDON, England
Goli la 'usiku' lililofungwa na Mikel Arteta mwishowe lilihitimisha ugumu wa klabu ya mkiani mwa msimamo wa ligi ya QPR wakati Arsenal ilipojipoza kutokana na matokeo mabaya waliyopata katikati ya wiki kwa ushindi muhimu wa 1-0 katika Ligi Kuu ya England leo.
Arteta alifunga kwa shuti la karibu kabisa na lango, baada ya mpira wake wa kwanza aliopiga kichwa kugonga 'besela' langoni mwa QPR, wakati Arsenal ikirejea kwenye mstari baada ya vipigo viwili mfululizo walivyopata kutoka kwa Norwich na Schalke.
Ushindi huo wa Arsenal iliyomiliki mpira kwa asilimia 70 ulipatikana baada ya Stephane M'Bia wa QPR kutolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia kosa lake la kumpiga teke Thomas Vermaelen wa Arsenal.
Esteban Granero wa QPR na mwenzake Jamie Mackie walipoteza nafasi za wazi kuisawazishia timu yao.
Kiungo wa timu ya taifa ya England, Jack Wilshere alicheza kwa dakika 67 wakati alipoichezea timu ya wakubwa ya Arsenal kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje kwa miezi 17 kutokana na majeraha.
Hata hivyo, ushindi huo haukuisadia Arsenal kupanda zaidi bali imebaki katika nafasi yake ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kufikisha pointi 15; huku Chelsea (pointi 22), Man U (pointi 19) na Man City (pointi 18) zikiendelea kushika nafasi tatu za juu.
Matokeo mengine ya mechi za leo za Ligi Kuu ya England:
• Aston Villa 1 - 1 Norwich
• Reading 3 - 3 Fulham
• Stoke 0 - 0 Sunderland
• Wigan 2 - 1 West Ham
MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND BAADA YA MECHI ZA LEO JIONI:
P
|
GD
|
Pts
|
||
Iko palepale 1
|
8
|
13
|
22
|
|
Imepanda 2
|
9
|
8
|
19
|
|
Imeshuka 3
|
8
|
10
|
18
|
|
Iko palepale 4
|
9
|
8
|
15
|
|
Iko palepale 5
|
8
|
6
|
15
|
|
Iko palepale 6
|
9
|
5
|
14
|
|
Iko palepale 7
|
8
|
3
|
14
|
|
Iko palepale 8
|
8
|
3
|
14
|
|
Iko palepale 9
|
9
|
2
|
14
|
|
Iko palepale 10
|
9
|
2
|
12
|
|
Iko palepale 11
|
8
|
-3
|
10
|
|
Iko palepale 12
|
9
|
-1
|
9
|
|
Iko palepale 13
|
8
|
-2
|
9
|
|
Iko palepale 14
|
8
|
-2
|
9
|
|
Iko palepale 15
|
9
|
-6
|
8
|
|
Iko palepale 16
|
9
|
-11
|
7
|
|
Iko palepale 17
|
9
|
-7
|
6
|
|
Iko palepale 18
|
8
|
-6
|
4
|
|
Iko palepale 19
|
8
|
-11
|
4
|
|
Iko palepale 20
|
9
|
-11
|
3
|
No comments:
Post a Comment