Saturday, October 27, 2012

CARLOS TEVEZ AFUNGA BAO KALI LILILOWAPA USHINDI WA 1-0 DHIDI YA SWANSEA CITY.... SASA WAPAA NA KUKAMATA NAFASI YA PILI KWENYE MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND


Goooooohhhhh....! Carlos Tevez wa Man City akishangilia goli alilofunga dhidi ya Swansea wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester leo Oktoba 27, 2012.
Carlos Tevez wa Man City akikokota mpira wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Swansea leo, Oktoba 27, 2012.
Yaya Toure wa Manchester City akimtoka na Pablo Hernandez wa Swansea City wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester leo Oktoba 27, 2012. 
Mario Balotelli wa Manchester City akitafuta mbinu za kumfunga kipa Michel Vorm wa Swansea City wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester leo Oktoba 27, 2012.
Samir Nasri wa Man City akimtoka beki wa Swansea wakat wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester, leo Oktoba 27, 2012.
Mario Balotelli wa Manchester City akimlamba chenga Wayne Routledge wa Swansea City wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester leo Oktoba 27, 2012.
Sergio Aguero wa Manchester City akichuana na Ki Sung- Yeung wa Swanseawakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester leo, Oktoba 27, 2012. 
MANCHESTER, England
Goli safi la ushindi lililofungwa na Carlos Tevez liliisaidia Manchester City iliyocheza 'kichovu' kupata ushindi wa nyumbani wa 1-0 katika mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Swansea City kwenye Uwanja wa Etihad Stadium usiku huu.

Tevez alifunga goli hilo kwa shuti kali la umbali wa mita 25 katika dakika ya 61 ya mechi ambayo iliongezwa dakika 12 na sekunde 42 za majeruhi na kuandika historia ya muda mrefu zaidi kuwahi kuongezwa baada ya kumlizika kwa dakika 90 za kawaida katika Ligi Kuu ya England.

Kuongezwa kwa dakika hizo kulitokana na kuumia kwa kipa wa Swansea, Michel Vorm, aliyekuwa akijaribu kuokoa shuti la Tevez lililomshinda hata hivyo na kujaa wavuni, na beki Micah Richards wa Man City aliyeumia goti na kupata jeraha linaloonyesha kuwa hataonerkana tena uwanjani katika sehemu yote iliyobaki ya msimu.

Baada ya kuchapwa katikati ya wiki kwenye mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Ajax, ushindi huu uliashiria kurejea katika kasi ya ushindi kwa Man City lakini timu hiyo ya kocha Roberto Mancini inayojaribu kutetea ubingwa wa England ilionyesha kiwango cha chini na kuusaka mpira kwa 'tochi' katika muda mwingi wa mechi.

Siku tatu baada ya kupata kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Ajax mjini Amsterdam, City ilipelekeshwa kipindi cha kwanza, na kuo0nekana ikikosa mbinu za ushindi.

Maelfu ya mashabiki wenye tiketi za msimu za Man City waliamua kutofika uwanjani. Labda kutokana na baridi kali au kutokana na ukweli kwamba mechi hiyo ilionyeshwa kupitia TV - au labda walijua kwamba timu yao itacheza 'kichovu'.

Kama ilivyokuwa Ajax, Swansea walionyesha soka safi na kuwabana katika muda mwingi wa mechi, lakini walishindwa kutumia nafasi walizopata na pia kukwazwa na ukuta wa Man City ambao muda mwingi walionekana kujihami kwa 'kuweka basi'.

Kikosi cha Mancini kilihaha hadi katika dakika ya 38 ndipo kilipopata nafasi ya kupiga shuti la kwanza lililolenga goli kutokana na jitihada binafsi za Carlos Tevez.

Nafasi nzuri zaidi ya kufunga katika kipindi cha kwanza ilipotezwa na straika wa Swansea, Michu, aliyekimbilia pasi safi aliyochomekewa lakini akashindwa kufunga baada ya shuti lake kuzuiwa na kipa Joe Hart.

Kwa ushindi walioupata, Man City walipanda hadi katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kufikisha pointi 21, mbili zaidi ya Man U na moja kabla ya kuwashika vinara Chelsea ambao kesho Jumapili watavaana na Man U.


Matokeo mechi nyingine za Ligi Kuu ya England zilizochezwa leo Jumamosi Oktba 27, 2012:


•    Aston Villa 1 - 1 Norwich 
•  Arsenal         1 - 1   QPR
•    Reading     3 - 3 Fulham
•    Stoke         0 - 0 Sunderland 
•    Wigan        2 - 1 West Ham 



MSIMAMO LIGI KUU ENGLAND BAADA YA MECHI ZA LEO


P 
GD
Pts

1
8
13
22
2
9
9
21
3
8
10
18
4
9
8
15
5
8
6
15
6
9
5
14
7
8
3
14
8
8
3
14
9
9
2
14
10
9
1
11
11
8
-3
10
12
9
-1
9
13
8
-2
9
14
8
-2
9
15
9
-6
8
16
9
-11
7
17
9
-7
6
18
8
-6
4
19
8
-11
4
20
QPR
9
-11

No comments:

Post a Comment