Wednesday, October 10, 2012

MHE. LOWASA ATEMBELEWA LEO JIMBONI KWAKE MONDULI NA VIMWANA WATAKAOSHIRIKI REDD'S MISS TANZANIA 2012

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mhe. Edward Lowassa akisalimiana na msimamizi (Matron) wa warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012, Irene Karugaba wakati Warembo hao walipotembelea Nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Monduli ili kupata baraka zake. Mhe. Lowassa aliwapokea warembo hao kwa furaha na kuzungumza nao machache juu ya mafanikio ya Mashindano hayo na Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania.
Mungu amewapendelea kwa uzuri na bashasha... Mhe. Lowassa akiteta na warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012 leo.

Karibuni sana na mjisikie mpo nyumbani...! Mhe. Lowassa akiendelea kuwapa nasaha zake warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mhe. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa kenye picha ya pamoja na Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2012 pamoja na Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania. (Picha Zote kwa Hisani ya Intellectuals Communications Limited)

No comments:

Post a Comment