Wednesday, October 10, 2012

HIGUAIN: SIPENDI KUWALINGANISHA CRISTIANO RONALDO NA LIONEL MESSI... WOTE WAWILI NI WAKALI BALAA...!

Messi, Higuain na Di Maria

Messi na Higuain

Higuain na Ronaldo

Higuain na Ronaldo

Higuain na Ronaldo wa Real Madrid wakishangilia goli
BUENOS AIRES, Argentina
Mabishano kuhusiana na nani anastahili tuzo ya Mwansoka Bora wa Dunia kuhusiana na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo yako kila mahala duniani.

Sakata hilo lilitwaa nafasi tena katika kambi ya timu ya taifa ya Argentina. Kuna mchezaji mmoja ambaye ana bahati ya kucheza pamoja na nyota hao wawili wa dunia katika ngazi ya klabu (Real Madrid) na timu ya taifa (Argentina), ambaye ni Higuaín.

Yeye anatoa jibu la kidiplomasia kuhusiana na swali kwamba nani kati ya wawili hao ni anastahili tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia.

"Nina bahati ya kucheza pamoja na wote wawili --  Messi na Cristiano -- na sipoendi kuwalinganisha. Ni wachezaji wawili ambao hufanya mambo makubwa kiasi cha kustahili kuitwa kuwa ni wanasoka bora zaidi wa dunia," amesema Higuain a.k.a 'El Pipita'.

Higuaín na Di María walitua katika kambi ya timu ya taifa ya Argentina Jumanne kujiandaa na mechi zao za kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay na Chile.

Straika huyo alitua Argentina baada ya kupoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid mbele ya Benzema, aliyeanza katika mechi za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Ajax na ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Barcelona.

'El Pipita' amepata nafsi ya kujipoza kwa kuanza katika kikosi cha Argentina kwani ni wazi kwamba kocha wao, Alejandro Sabella atataka kumchezesha na wakali wenzake Leo Messi, Sergio Agüero na Ángel Di María, waliotengeneza ushirikiano uliopachikwa jina la 'the fantastic four'.

No comments:

Post a Comment