Wednesday, October 10, 2012

JOKATE AZINDUA KIDOTI BRAND

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Tanzania Limited, Jokate Mwegelo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa lebo yake ya Kidoti kwenye hoteli ya Serena.

Jokate Mwegelo akizungumza wakati wa kuzindua mtandao wake wa mavazi na urembo wa Kidoti

Jokate Mwegelo akiwa na wanamitindo waliovaa nywele za mtandao wake wa Kidoti wakati wa uzinduzi mtandao wake wa mavazi na urembo
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Tanzania Limited, Jokate Mwegelo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa lebo yake ya Kidoti kwenye hoteli ya Serena.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Tanzania Limited, Jokate Mwegelo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa lebo yake ya Kidoti kwenye hoteli ya Serena.
Jokate Mwegelo akiwa na wanamitindo waliovaa nywele za mtandao wake wa Kidoti wakati wa uzinduzi mtandao wake wa mavazi na urembo
Jokate Mwegelo akiwa na wanamitindo waliovaa nywele za mtandao wake wa Kidoti wakati wa uzinduzi mtandao wake wa mavazi na urembo

MISS Tanzania namba mbili wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo amezindua rasmi lebo yake ya mitindo ya nywele na nguo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Brand.

Jokate ambaye alianza kujihusisha na masuala ya mitindo mwaka jana, alizindua lebo yake hiyo kwenye hoteli ya Serena na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wa masuala ya urembo, maonyesho ya mavazi, wanamitindo na wauzaji wa bidhaa hizo kutoka kila kona ya jiji.

Alisema kuwa hatua ya kuamua kuanzisha lebo hiyo ni moja ya mikakati yake ya kujitafutia fedha kama mjasiriamali na lengo lake kubwa ni kutaka kusimama yeye mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu.

Alifafanua kuwa kabla ya kuanzisha lebo na kampuni yake, alifanya utafiti wa hali ya juu kuhusiana na sekta hiyo na hatimaye kushiriki kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya mavazi ya Red Ribbon na sasa kuamua kwenda mbali zaidi kwa kuingia katika fani ya nywele ambazo anatengeneza yeye mwenyewe.

Amesema kuwa mbali ya kushiriki katika maonyesho mbali mbali, pia atakuwa anasambaza bidhaa zake za nywele na nguo kwenye maduka mbali mbali ili kuwawezesha wananchi kutumia bidhaa zake.

“Lengo langu kubwa ni kutawala soko na kuwa milionea, hiyo ndiyo ndoto yangu pamoja na kuuza bidhaa zangu hasa za nywele kuanzia Sh. 9,500 na Sh. 12,000. Nguo za Kidoti zitatambulishwa rasmi katika soko mwakani (2013) zikifuatiwa na vifuasi vya urembo pamoja na vipodozi,” alisema Jokate.

Alisema kuwa  msingi wa ubunifu wake ni mchanganyiko wa kipekee wa kiini cha utamaduni wa Kiafrika pamoja na mitindo ya kisasa ulimwenguni kwa ajili ya wanawake na wanaume wa kisasa.

No comments:

Post a Comment