Sunday, October 21, 2012

MESSI APIGA 'HAT-TRICK', ABAKISHA MAGOLI MANNE KUIFIKIA REKODI YA WAKATI WOTE YA PELE

Straika wa Barcelona, Lionel Messi akishangilia goli lake la pili dhidi ya Deportivo Coruna wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Riazor mjini Coruna jana usiku Oktoba 20, 2012. Picha: REUTERS

Carlos Marchena (kushoto) wa Deportivo Coruna akiwania mpira dhidi ya straika wa Barcelona, Lionel Messi wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Riazor mjini Coruna jana usiku Oktoba 20, 2012. Picha: REUTERS

Nelson Oliveira (kushoto) wa Deportivo Coruna akiwania mpira dhidi ya kiungo wa Barcelona, Sergio Busquets wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Riazor mjini Coruna jana usiku Oktoba 20, 2012. Picha: REUTERS
Safari hiyo... Straika wa Barcelona, Lionel Messi akimtoka mchezaji wa Deportivo Coruna, Carlos Marchena (kushoto) wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Riazor mjini Coruna jana usiku Oktoba 20, 2012. Picha: REUTERS
Straika wa Barcelona, Lionel Messi (kulia) akishangaa maamuzi ya refa Jose Luis Paradas Romero wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Riazor mjini Coruna jana usiku Oktoba 20, 2012. Picha: REUTERS

Beki wa Barcelona, Jordi Alba akishangilia goli lake dhidi ya Deportivo Coruna wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Riazor mjini Coruna jana usiku Oktoba 20, 2012. Picha: REUTERS

Straika wa Barcelona, Lionel Messi (kulia) akishangilia goli lake la pili dhidi ya Deportivo Coruna na mchezaji mwenzake Francesc Fabregas wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Riazor mjini Coruna jana usiku Oktoba 20, 2012. Picha: REUTERS
Straika wa Barcelona, Lionel Messi akishangilia goli lake la pili dhidi ya Deportivo Coruna wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Riazor mjini Coruna jana usiku Oktoba 20, 2012. Picha: REUTERS

Winga wa Barcelona, Cristian Tello akishangilia goli lake dhidi ya Deportivo Coruna wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Riazor mjini Coruna jana usiku Oktoba 20, 2012. Picha: REUTERS
Beki wa Barcelona, Jordi Alba akishangilia goli lake dhidi ya Deportivo Coruna wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Riazor mjini Coruna jana usiku Oktoba 20, 2012. Picha: REUTERS


LIONEL Messi alifunga 'hat-trick' yake ya 15 ya La Liga katika mechi ngumu iliyozaa magoli tisa wakati Barcelona walipohaha kuziba pengo Javier Mascherano aliyetolewa kwa kadi nyekundu na kushinda 5-4 ugenini dhidi ya Deportivo Coruna na kupaa pointi tatu juu ya msimamo jana usiku.

Kiwango cha juu ya Messi kiliyafunika matokeo ya Real Madrid ushindi wa 2-0 dhidi ya timu iliyopanda daraja ya Celta Vigo. Gonzalo Higuain na Cristiano Ronaldo (penalti) walifunga magoli hayo yaliyoiinua timu ya Jose Mourinho hadi katika nafasi ya nne ya msimamo, pointi nane nyuma ya mahasimu wao Barca.

Mwanasoka Bora wa Dunia Messi, ambaye alikuwa akitarajia kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza, alifikisha magoli 71 kwa klabu na timu yake ya taifa katika mwaka wa kalenda wa 2012 (yaani Januari hadi Desemba). Jambo hilo linamfanya abakishe magoli manne tu kuifikia rekodi ya wakati wote iliyowekwa na gwiji wa Brazil, Pele aliyefunga magoli 75 mwaka 1959.

Muargentina huyo amefunga magoli 11 katika mechi nane za La Liga msimu huu, mawili zaidi ya Ronaldo. Barca ambayo haijafungwa ina pointi 22, tatu juu Atletico Madrid ambao walitarajiwa kucheza mechi yao ya mkononi leo usiku ugenini dhidi ya Real Sociedad.

"Yeye (Messi) ameondoka kwenda hospitali hivi sasa kwa sababu mkewe anakaribia kujifungua," mkurugenzi wa michezo wa Barca, Andoni Zubizarreta aliiambia televisheni ya Hispania.

Malaga ni wa tatu katika msimami wakiwa na pointi 17 baada ya Joaquin kusahihisha makosa yake ya kukosa penalti kwa kufunga goli la ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Real Valladolid.

Barca walionekana kuelekea kupata ushindi wa saba wakati walipopata uongozi wa magoli 3-0 ndani ya dakika 18 za kwanza kwenye uwanja wa Deportivo wa Riazor Stadium.

Jordi Alba alikimbilia kwa kasi pasi ya Cesc Fabregas na kufunga goli katika dakika ya tatu, Cristian Tello akaongeza la pili na kisha Messi akafunga lake la kwanza juzi usiku kufuatia pasi akili ya kisigino kutoka kwa Fabregas.

Wenyeji walipunguza magoli mawili tofauti na mwelekeo wa mechi kupitia kwa Pizzi (penalti) na Alex Bergantinos kabla ya Messi kuitumia vyema pasi ya nyingine ya Fabregas na kufanya matokeo yawe 4-2 wakati wa mapumziko.

Katika mwanzo mzuri wa kipindi cha pili kwa wenyeji, kiungo Pizzi alipiga bonge la 'fri-kiki' lililokwenda moja kwa moja wavuni katika dakika ya 47 na Mascherano akatolewa kwa kadi nyekundu ambayo ilionekana haikustahili dakika mbili baadaye.

Kocha wa Barca, Tito Vilanova alimtoa Fabregas na kumuingiza Xavi kabla ya Messi, ambaye pia aligongeza nguzo ya goli kwa 'fri-kiki' kali, alionekana kama amemaliza mechi hyo pale alipofanya matokeo yasomeke 5-3 kufuatia staili yake maarufu ya juhudi binafsi kwa kuwalamba chenga mabeki na kufunga kiufundi katika dakika ya 77.

Goli la ajabu la kujifunga kutoka kwa beki wa kushoto wa Barca, Jordi Alba, wakati alipomtungua kipa wake Victor Valdes kutokea ndani ya boksi wakati akijaribu kumiliki mpira wa krosi, na kuwapa Depor matumaini mapya lakini hawakuweza kuzinduka licha ya kuliandama lango la Barca waliobaki 10 uwanjani.

No comments:

Post a Comment