Sunday, October 21, 2012

TP MAZEMBE YA KINA MBWANA SAMATTA YANG’OLEWA LIGI YA KLABU BINGWA AFRIKA… NI BAADA YA KUCHAPWA 1-0 NA ESPERANCE KATIKA MARUDIANO NUSU FAINALI…!


Mtanzania Mbwana Samatta wa TP Mazembe (kushoto) akimtoka beki Khalil Chemmam wa Esperance ya Tunisia wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika kwenye Uwanja wa Rades mjini Tunis, jana Oktoba 20, 2012. (Picha: REUTERS)

TUNIS, Tunisia
Goli la kipindi cha pili kutoka kwa Mohamed Ben Mansour liliwapa Esperance ushindi wa nyumbani wa 1-0 dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati mabingwa hao watatezi wakitinga fainali kwa msimu wa tatu mfululizo.

Beki huyo alifunga wakati zikiwa zimebaki dakika 20 kabla mechi kumalizika na kuipa Esperance nafasi ya kutetea taji hilo lenye hadhi ya juu zaidi kwa ngazi ya klabu barani Afrika.
Esperance wametinga fainali kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0 baada ya kulazimisha sare ya 0-0 katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Mazembe iliyochezwa nchini Kongo.

Sasa Esperance watacheza fainali na mshindi wa mechi ya leo itakayochezwa jijini Cairo kati ya Ahly ya Misri au Sunshine Stars ya Nigeria.

Esperance waliishambulia zaidi Mazembe katika kipindi cha kwanza na kukaribia kufunga mara kadhaa, ikiwa ni pamoja na mpira wa kichwa uliogonga besela katika dakika ya 37 kutoka kwa
Youssef Msakni.

Nyota wa Mazembe, akiwamo straika wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta walifanya mashambulizi kadhaa ya kustukiza kwa nia ya kurudisha goli hilo lakini bahati haikuwa yao.  Basisila Lusadisu alipata nafasi nzuri ya kufunga lakini akapiga shuti lililomlenga kipa wa Esperance ambaye alifanya kazi nyepesi ya kupangua.

No comments:

Post a Comment