Thursday, October 11, 2012

NANI KUAGA EPIQ BSS WIKI HII?


Majaji wa Epiq BSS wakifuatilia shindano hilo la kusaka vipaji vya kuimba. Kutoka Kushoto ni Master Jay, Ritha Paulsen na Salama Jabir

SHINDANO la Epiq BSS limezidi kupamba moto, kwani kile kipindi kigumu cha washiriki kutoka kinakaribia tena ambapo Jumapili hii tutashuhudia washiriki wengine wawili kati ya kumi wakiaga mashindano hayo.

Washiriki walio kwenye hatari hiyo ama kwa jina maarufu kwa wapenzi wa shindano hilo “Rocha Rocha” ni pamoja na Menyanah Atiki mshiriki mwenye namba za ushiriki EBSS 04, Linias Mhaya mwenye namba EBSS 03, Norman Severino mwenye EBSS 05, pamoja na mshiriki mwingine mwenye namba za ushiriki EBSS 01 Godfrey Kato, ambaye wiki iliyopita alikuwa kwenye hatihati hiyo lakini alinusurika baada ya kupata kura nyingi za kubaki.

Wiki iliyopita tulishuhudia washiriki wakitoka, kati ya wale kumi na mbili waliofanikiwa kuingia mjengoni ambao ni Vincent Mushi pamoja na mshiriki mwenzie Salma Mahini.

Kwa upande wake jaji mkuu wa Epiq BSS, Madam Ritha Paulsen, ameendelea kusisitiza watu wapige kura kwa wingi ili kuwaokoa washiriki wanaowapenda.

“Bila kura yako mshiriki unayempenda atatoka, shindano hili sasa liko kwenu nyie mashabiki kuchagua mshindi mnayemtaka,” alisema Madam Ritha.

Ili kuwaokoa washiriki wasitoke kwenye jumba unaweza kupiga kura kwenda EBSS unaacha nafasi kisha unaandika namba ya mshiriki kwenda namba 15530.

No comments:

Post a Comment