Sunday, October 28, 2012

LIONEL MESSI APIGA 2 WAKATI BARCA IKIIUA RAYO VALLECANO 5-0... MESSI SASA AFIKISHA MABAO 301 KATIKA MECHI 419... ABAKIZA GOLI MBILI TU KUFIKIA REKODI YA MBRAZILI PELE YA MABAO 75 KWA MWAKA MMOJA WA KALENDA ILIYODUMU TANGU MWAKA 1959....!

Asante Mungu...! Messi akishangilia moja kati ya mabao yake mawili wakati walipocheza dhidi ya Rayo Vallecano mjini Madrid leo Oktoba 27, 2012

Lionel Messi (kulia) akimpiga chenga kipa waRayo Vallecano kabla ya kwenda kufunga wakati  wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania, leo Oktoba 27.


Kipa wa Rayo Vallecano akijaribu bila mafanikio kumzuia Messi wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Hispania leo, Oktoba 27, 2012

Xavi wa Barcelona akishangilia baada ya kufunga dhidi ya Rayo Vallecano wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Hispania leo, Oktoba 27, 2012.

Unatisha mkuu...! Cesc Fabregas akipongezana na Xavi


Messi akip[ongezwa na wenzake baada ya kufunga goli la pili kwake.

Messi akimpongeza beki chipukizi, Montoya baada ya kumpa pasi safi iliyozaa goli.

Goooohhhh...! Barca wakifurahia ushindi mnono wa 5-0 dhidi ya Rayo Valecano leo Oktoba 27.

David Villa akishangilia goli alilofunga dhidi ya Rayo.
MADRID, Hispania
LIONEL Messi alivuka idadi yake binafsi ya jumla ya magoli 300 kwa kufunga magoli mawili wakati Barcelona ikiisambaratisha Rayo Vallecano mabao 5-0 mjini Madrid usiku huu wa Jumamosi (Oktoba 27, 2012) na kujichimbia kileleni mwa msimamo wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania kwa tofauti ya pointi tatu.

David Villa, Xavi Hernandez na Cesc Fabregas walifunga magoli mengine kila mmoja na hivyo kuzidi kuiacha Atletico Madrid inayokamata nafasi ya pili na ambayo kesho Jumapili (Oktoba 28, 2012) itacheza dhidi ya Osasuna.

Mabao ya Messi yalikuwa ni ya 300 na 301 tangu aanze rasmi kucheza soka la kulipwa, kati ya hayo akifunga mabao 270 kwa klabu yake ya Barca na 31 kwa timu yake ya taifa ya Argentina huku hadi sasa akicheza jumla ya mechi 419 tu.

Mabao hayo pia yalimfanya Messi afikishe mabao 13 katika La Liga msimu huu na 73 ya michuano yote kwa mwaka wa kalenda wa 2012.

Idadi ya mabao hayo pia imemfanya Messi abakize magoli mawili tu ili kuifikia rekodi ya Pele ya jumla ya mabao 75 aliyoifungia klabu yake ya Santos na timu ya taifa ya Brazil mwaka 1959, na pia amebakiza mabao 12 tu kuifikia rekodi bora ya muda wote katika kipindi cha mwaka wa kalenda ya magoli 85 iliyowekwa na Gerd Mueller wakati akizichezea Bayern Munich na timu yake ya taifa ya Ujerumani Magharibi mwaka 1972.

Rayo walianza vizuri na madai yao ya kutaka penati yalikataliwa na refa katika dakika ya nane wakati Fabregas aliponekana akimvuta kwa nyuma Leo Baptistao.

Rayo waliishambulia Barca na hali iliendelea hivyo katika dakika ya 19 wakati Messi alipopiga shuti la kwanza la Barca kuelekea langoni mwa Vallecano lakini mpira ukatoka nje.

Hata hivyo, dakika moja baadaye, Barca walipata bao la utangulizi kupitia kwa David Villa aliyetumia vyema pasi ya Cesc Fabregas.

Messi aliongeza bao la pili katika dakika ya 47. Xavi na Fabregas baadaye wakafunga magoli mengine mawili zaidi wakati zikiwa zimebaki dakika 10 kabla mechi kumalizika.

Dakika mbili kabla mechi kumalizika, Messi aliiwahi pasi safi ya Fabregas na kufunga goli lake la pili na la tano la Barcelona dhidi ya Rayo Vallecano.


MATOKEO MECHI NYINGINE  LA LIGA, LIGI KUU YA HISPANIA LEO J'MOSI OKT. 27:
   Espanyol          0 - 0  Malaga
   Real Betis        1 - 0  Valencia
   Celta de Vigo   1 - 1  Deportivo
   

MSIMAMO WA LA LIGA, LIGI KUU YA HISPANIA BAADA YA MECHI ZA J'MOSI OKT. 27 

                                     P    GD    Pts      
1 Barcelona                   9    18      25      
2 Atl Madrid                 8    11       22      
3 Malaga                       9     8       18      
4 Real Betis                   9     0        16      
5 Real Madrid                8     9       14      
6 Sevilla                         8     2        14      
7 Levante                       8    -4       13      
8 Mallorca                      8     1       11      
9 Valencia                       9    -1        11      
10 Valladolid                   8     3        10      
11 Celta de Vigo             9    -1        10      
12 Getafe                        8    -3        10      
13 Rayo Vallecano           9    -11      10      
14 Real Zaragoza             8    -3          9      
15 Real Sociedad             8    -4          9      
16 Granada                      8    -5          8      
17 Athletic Bilbao             8     -6         8      
18 Deportivo                     9    -6         7      
19 Espanyol                       9    -4         6      
20 Osasuna                        8    -4         5    

No comments:

Post a Comment