Gooooh...! Cristiano Ronaldo akishangilia goli lake la kwanza dhidi ya Real Mallorca wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania leo Oktoba 28, 2012. |
Natishaaaa....! Nyota wa mchezo, Gonzalo Higuain akishangilia goli lake la kwanza wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania |
Safi sana... niletee pasi nyingine kali ya goli na lazima nitafunga. Ronaldo wa Real Madrid (kulia) akipongezana na Gonzalo Higuain wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Englandf leo Oktoba 28, 2012. |
Sergio Ramos (kushoto) akimpongeza Ronaldo baada ya kufunga goli dhidi ya Real Mallorca wakatri wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania. |
Gonzalo Higuaon akishangilia goli lake la pili dhidi ya Real Mallorca |
Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia goli lao la tano lililowahakikishia ushindi mnono wa 5-0 dhidi ya Real Mallorca kwenye Uwanja wa Iberostar, leo Oktoba 28, 2012. |
Falcao akiruka juu kuwahi mpira usitue kwa mabeki wa Osasuna wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania leo Oktoba 28, 20-12. |
Kama Messi vile...! Falcao akiwatoka mabeki wa Osasuna wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania leo Oktoba 28, 2012. |
Radamel Falcao akishangilia baada ya kumtungua kipa ... wa Osasuna wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania leo Oktoba 28, 2012. |
Real Madrid walirejea katika kasi yao ya ushindi kwa kuishindilia Real Mallorca mabao 5-0 wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania iliyochezwa usiku huu wa Jumapili kwenye Uwanja wa Iberostar.
Baada ya wiki mbaya waliyopata kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Borussia Dortmund kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Real walionysha kiwango cha juu kuanzia mwanzo wa mechi hadi mwisho, na kutwaa pointi zote tatu.
Gonzalo Higuain alifunga goli la utangulizi katika dakika ya nane tu ya mechi hiyo akitumia pasi safi iliyombabatiza beki ya Angel Di Maria, kabla Cristiano Ronaldo hajaongeza la pili katika dakika ya 22 akitumia vyema pasi ya goli kutoka kwa Higuain.
Wawili hao waliwaliza tena wenyeji katika kipindi cha pili, wakati Higuain alipofunga goli la tatu katika dakika ya 70 akitumia pasi ya Ronaldo, huku Ronaldo naye akiongeza la nne dakika tatu baadaye kufuatia pasi nyingine kali ya Huguain.
Mtokea benchi Jose Callejon alifanya ubao wa magoli usomeke 5-0 wakati alipofunga jingine katika dakika za majeruhi, wakati Real Madrid ikipaa hadi katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa La Liga, ingawa bado imeachwa na vinara Barcelona kwa tofauti ya pointi nane.
Katika mechi nyingine leo, straika wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao alifunga goli safi na kuisaidia Atletico Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Osasuna.
Goli alilofunga Falcao ni la 10 kwake katika msimu huu wa La Liga, akizidiwa na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid aliyefikisha magoli 11 na Lionel Messi wa Barcelona aliyefikisha magoli 13.
Ushindi huo wa nane mfululizo uliendelea kuiweka Atletico Madrid kileleni mwa msimamo wa Lag Liga, ikizidiwa na vinara Barcelona kwa tofauti ya pointi nane.
MATOKEO MECHI NYINGINE ZA LEO KATIKA LA LIGA, LIGI KUU HISPANIA
Real Zaragoza 2 - 1 Sevilla
Levante 3 - 1 Granada
Athletic Bilbao 1 - 2 Getafe
Atletico Madrid 3 - 1 Osasuna
Mallorca 0 - 5 Real Madrid
No comments:
Post a Comment