Monday, October 8, 2012

KUMLINGANISHA RONALDO NA MESSI IWE MARUFUKU - MOURINHO

Ronaldo akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya barcelona kwenye Uwanja wa Nou Camp jana usiku.

KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amewasifu Cristiano Ronaldo na nyota wa Barcelona, Lionel Messi baada ya wawili hao kufunga mara mbili kila mmoja katika sare ya 2-2 juzi usiku na ametaka ipigwe marufuku kuwalinganisha. 

Alipoulizwa nani anapaswa kutwaa tuzo ya Ballon d'Or ya mwanasoka bora wa dunia, alisema: "Sitaki kuiwaza sana hiyo. 

"Nadhani ipigwe marufuku sasa kusema nani ni mwanasoka bora wa dunia kwa sababu hawa wawili ni wa sayari nyingine. 

"Ningependa mchezaji wangu ashinde kwa sababu yeye ni bingwa wa ligi bora duniani, lakini nadhani wote ni wachezaji wazuri sana."

No comments:

Post a Comment