Monday, October 8, 2012

DANI ALVES NJE WIKI 3

Daniel Alves

BARCELONA imethibitisha kwamba beki Daniel Alves atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu.


Mbrazili huyo aliumia misuli ya nyuma ya paja wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Real Madrid iliyomalizika kwa sare ya 2-2 juzi. Magoli mawili ya Barcelona yalifungwa na Lionel Messi wakati mawili ya Real yalifungwa na Cristiano Ronaldo kwenye Uwanja wa Nou Camp mjini Barcelona.

Alves alikuwa ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya Iraq na Japan Oktoba 11 na 16, lakini sasa atakosa mechi hizo za wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment