Wednesday, October 10, 2012

BAUNSA LILILOWAHI KUMLINDA LIONEL MESSI LADAI KUWAHI KUWA JAMBAZI NA KUPORA KATIKA BENKI 500!

Kutoka kulia ni baunsa wa zamani wa Lionel Messi, Daniel Rojo, Messi mwenyewe, muimbaji wa Argentina Andrés Calamaro na Javier Mascherano wakifurahi wakati wakipozi kwa picha ya pamoja.
Daniel Rojo akiwa katika maeneo ya Barcelona. 
BARCELONA, Hispania
Barcelona waliwahi kuajiri bodigadi wa kumlinda Lionel Messi aliyekuwa na rekodi ya kutisha ya kuwahi kufanya uporaji katika benki MIA TANO!

Baunsa huyo aitwaye Daniel Rojo amezungumzia maisha yake katika kipindi chote cha kumlinda Messi na kufichua mengi kuhusiana na maisha yake wakati akihojiwa na Gazzetta dello Sport.

"Katika maisha yangu nimewahi kufanya uporaji kwenye benki 500. Nilipenda sana maisha ya juu, magari na nguo za bei mbaya, na dawa za kulevya. Nilianza wakati nikiwa na miaka 15 na baadaye nikawa mtaalam," alifichua Rojo.

“Mwaka 1997 niliamua kubadili maisha yangu na kujiunga na dunia ya soka. Mwaka 2006 nilianza kufanya kazi Barcelona. Wakati huo, (Frank) Rijkaard alikuwa ndiye kocha na timu ilinituma kuwafuata wachezaji waliokuwa wakilewa sana katika klabu za usiku na kushindwa kuendesha.”

Kuhusu Messi, Rojo aliendelea: “Siku moja walinituma kumfuata baada ya mazoezi. Messi ni mtoto mpole na wakati akila alikuwa akikaa kando yangu huku mimi nikimsimulia maisha yangu. Hakuwa na mengi ya kusema, katika maisha yake hakuwa akifanya jambo jingine lolote mbali na mazoezi na kucheza soka. Hawakumruhusu pia kwenda kujirusha na wasichana, ni hivi sasa tu ndipo amejua maisha yanamaanisha nini."

Aliendelea: “Sijafanya nao kazi kwa miaka kadhaa sasa lakini mara moja moja huwa tunakutana njiani. Mwaka uliopita nilikwenda kuangalia mechi ya Barcelona na rafiki zangu na kukutana na Leo aliyekuwa ameambatana na akina dada wawili warembo sana. Baadaye, nilitambua kwamba mmoja alikuwa mpenzi wake, Antonella Roccuzzo, na mwingine alikuwa ni mke wa (Javier) Mascherano na tukatoka wote kwenda kula. Mwishoni, Leo alinirudisha nyumbani kwangu huku nikiwa nimeketi kiti cha nyuma."

No comments:

Post a Comment