Friday, October 12, 2012

CASILLAS AFUKUZIA KUVUNJA REKODI YAKE LEO

Iker Casillas

Iker Casillas

Iker Casillas

Iker Casillas wa Hispania akiokoa mpira mbele ya mchezaji mwenzake Sergio Ramos huku Mario Balotelli (kulia) wa Italia akijaribu kufunga goli kwa kichwa wakati wa mechi ya fainali ya UEFA Euro 2012 kwenye Uwanja wa Olympic mjini Kiev, Ukraine Julai 1, 2012. Hispania walishinda 4-0 na kutwaa ubingwa.

Iker Casillas (katikati) wa Hispania akiokoa mpira mbele ya mchezaji mwenzake Sergio Ramos (kulia) huku Mario Balotelli wa Italia akijaribu kufunga goli kwa kichwa wakati wa mechi ya fainali ya UEFA Euro 2012 kwenye Uwanja wa Olympic mjini Kiev, Ukraine Julai 1, 2012. Hispania walishinda 4-0 na kutwaa ubingwa.

MAISHA ya kipa Iker Casillas kwa timu yake ya taifa ya Hispania yamekuwa ni yenye mfululizo wa kuvunja rekodi.

Kipa huyo tayari ameitwa 'mmoja wa wachezaji muhimu zaidi' katika miaka 92 ya historia ya timu hiyo ya taifa. Ugwiji wake unakua mechi hadi mechi, wakati Mhispania huyo akivunja takriban kila rekodi iliyo mbele yake.

Uwanja wa Dynama wa mjini Minsk, Belarus leo usiku unaweza kuwa mahala pengine pa kipa huyo kuweka rekodi nyingine ambayo haijavunjwa akiwa na fulana ya timu ya taifa ya Hispania. Ili jambo hili litimie, kipa huyo anahitaji kutoruhusu goli kwa dakika 77. Kama ataweza kufanya hivyo, ataivunja rekodi ya sasa ambayo inashikiliwa na… Casillas.

Hiyo inamaanisha kwamba kipa huyo anajiandaa kuivunja rekodi yake mwenyewe. Rekodi ya sasa ya kucheza dakika 715 bila ya kuruhusu goli - ambayo inaanzia kwenye goli alilofungwa Angelos Charisteas (wa Ugiriki) mwaka 2008 katika fainali za Mataifa ya Ulaya hadi goli aliloruhusu mjini Brussels mechi nane baadaye – inashikiliwa kwa pamoja na Casillas na Pepe Reina.

Hata hivyo, rekodi ya dunia kwa ngazi ya kimataifa iko mbali sana kufikiwa na nahodha huyo wa Real Madrid.

Dino Zoff bado ndiye anayeshikilia rekodi hiyo. Kipa huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Italia alicheza dakika 1,142 – yaani mechi 12 kamili mfululizo bila ya kuruhusu goli.

No comments:

Post a Comment