Friday, October 26, 2012

ETO'O ACHOCHEA UPYA BIFU NA ALEX SONG, ASEMA SONG SI MCHEZAJI MAARUFU HATA KWAO TU CAMEROON

Samuel Eto'o
Alex Song
Eto'o (kushoto) na Song

BIFU baina ya Samuel Eto'o na Alex Song ambalo lilionekana limemalizwa baada ya wawili hao kukutana hotelini na kumaliza tofauti zao, limeibuka upya kufuatia kauli iliyotolewa na Eto'o kumponda Song.

Wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha Ufaransa cha 'Canal Plus', Eto'o aliulizwa ni nini kilikuwa chanzo cha tofauti na staa mwenzake huyo wa Cameroon, naye alijibu: "Hakuna tofauti za mastaa za kuzizungumzia hapa, kwa sababu mimi ni mmoja wa wachezaji bora duniani na Song si bora hata nchini Cameroon."


Bifu baina ya wawili hao liliongezeka wakati wa fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini, na kuzaa kambi mbili zinazovutana ndani chumba cha kuvalia, ambapo baadhi ya wachezaji walimsapoti Eto'o wengine wakimsapoti Song.

Katika tukio hilo, Shirikisho la Soka la Cameroon liliingilia na kumtoza Song faini ya euro 1,500.

No comments:

Post a Comment