Sunday, October 21, 2012

DK. BILAL MGENI RASMI MKUTANO WA KIMATAIFA WA WAFANYABIASHARA WANAWAKE

Dkt. Mohamed Gharib Bilal

Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
MAKAMU wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Wanawake wafanyabiashara wa Nchi ya Mashariki mwa Afrika unaonza leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuimarisha mtandao wao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Fatma Riyami jana(leo) wakati  akiongea na waandishi  wa habari  Ofisi kwake.

Alisema kuwa Mkutano huo ambao ni wa saba(7) unafanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza tangu walionzisha ushirikiano huo wa wanawake wafanyabiashara kwa nchi za  Afrika Mashariki.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa wajumbe wa Mkutano huo wanatarajiwa kutoka katika Nchi za Kenya, Uganda, Rwanda , Burundi, Ethiopia , Sudan Kusini na mwenyeji Tanzania.

Alisema kuwa  Mkutano huo utakuwa fursa nzuri kwa wajumbe kutoka nchi zote saba kubadilishana uzoefu katika kazi ya kuwainua kiuchumi wakimama na kuimarisha Mtandao wa Wafanyabiashara wanawake katika Nchi za Afrika Mashariki.

“Mkutano huo utasaidia kuimarisha mtandao wa wafanyabiashara wanawake walioko katika Nchi hizo na hivyo kufanya soko la bidhaa zinatengeneza na wanawake wa pande hizo kuwa na soko kubwa,” alisisitiza Mwenyekiti huyo.

Aliongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kufanya soko la wafanyabiasha wanawake wa Afrika Mashariki kuwa kubwa na hivyo kuwainua kiuchumi wakimama.

Aidha Bibi Fatma Riyami alisema kuwa TWCC imeanzisha matawi katika Mikoa ya Kagera, Mwanza, Pwani, Dodoma, Mbeya, Dar es salaam na Arusha ikiwa na lengo la kutaka kuwa karibu na wafanfanyabiashara wanawake kwa nia kuimarisha Umoja wao.

No comments:

Post a Comment