Beki wa Real Madrid, Segio Ramos |
SAHAU kuhusu Cristiano Ronaldo au Lionel Messi, kura ya Iker Casillas kwa mwanasoka bora wa dunia 2012 inakwenda kwa kwa Sergio Ramos.
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Hispania anajiandaa kwenda kupiga kura ya mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or na, kwa mujibu wa gazeti la Sportyou, machaguo yake matatu ni Ramos, Cristiano na Xavi, kwa mtiririko huo.
Utaratibu wa kupiga kura unawaruhusu manahodha, makocha na waandishi wa habari kila mmoja kuwapa pointi wachezaji watatu, ambapo pointi 5 zinaenda kwa chaguo lake la kwanza, pointi 3 kwa jina lake la pili na 1 kwa chaguo la tatu.
Kwa maana hiyo Iker atampa pointi 5 Ramos, mchezaji mwenzake huyo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, ambaye alitwaa naye ubingwa wa 'La Liga' na taji la tatu la ubingwa wa Ulaya la timu ya taifa ya Hispania 2012.
Casillas ameamua kumpa heshima mmoja wa marafiki zake wa karibu, Ramos, ambaye amesaidia kumpa ulinzi mbele ya lango katika jezi nyeupe za Madrid na nyekundu za timu ya taifa ya Hispania.
Hii ni mara ya kwanza kwa kipa huyo wa timu ya taifa ya Hispania amempigia kura mchezaji mwenzake wa Hispania tangu utaratibu mpya wa kuchagua mshindi wa tuzo ya FIFA Ballon d'Or vkwa kupiga kura ulipoanzishwa 2010.
Ramos alikuwa nguzo muhimu katika mafanikio ya timu ya taifa ya Hispania katika kutwaa ubingwa wa Euro 2012, na Iker anaamini beki huyo mzaliwa wa Sevilla anastahili kutambuliwa kwa mchango wake. Beki huyo wa kati pia pia alifanya moja ya matukio makubwa ya michuano ya Euro 2012 pale alipofunga kiufundi penalti ya kudokoa mpira kwa staili maarufu kama "Panenka" dhidi ya Ureno.
Mwaka jana, chaguo la kwanza la Casillas lilikuwa ni Cristiano, ambaye sasa nahodha huyo wa Real Madrid amemshusha mshambuliaji wake hadi nafasi ya pili mara hii. Chaguo la tatu la Iker ni Xavi, ambaye anabaki kuwa mmoja wa rafiki zake wakubwa, licha ya uhasama uliopo katika mechi za karibuni za 'Clasico'.
No comments:
Post a Comment