Saturday, October 13, 2012

BENZEMA: DAIMA NAMUIGA RONALDO LIMA

Karim Benzema

Ronaldo de Lima

KARIM Benzema yuko katika kiwango kizuri klabuni kwake Real Madrid hivi sasa. Baada ya kuanza msimu ambao alipokwa namba yake na HiguaĆ­n katika kikosi cha kwanza cha Real, Mfaransa huyo amerejesha namba yake katika safu ya mashambulizi ya Madrid, akifunga magoli muhimu dhidi ya Manchester City, Rayo Vallecano na Ajax. Katika mahojiano na UEFA.com, straika huyo ameelezea dhamira yake ya kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na kuongeza ubora wake.

"Malengo yangu ni daima kuongezeka ubora kila siku. Nina bahati kuchezea timu kubwa. Nahitaji kuwa na msimu mzuri, kama niliokuwa nao mwaka jana, pamoja na kucheza vyema katika timu yangu ya taifa. Ni kipi ninachokosa ili kuwa mwanasoka bora? Sijui. Nafanya kazi kwa juhudi kuwa mwanasoka bora na sitasimama kujituma kuelekea huko," Benzema alisema.

Mbinu za ushambuliaji za Mfaransa huyo daima zimekuwa zikifananishwa na za Mbrazil Ronaldo. Mfaransa huyo ameelezea jinsi anavuomzimia mchezaji huyo wa zamani wa Madrid: "Katika msimu wangu wa kwanza Madrid nilipata fursa ya kukutana naye. Nimekuwa nikimfuatilia tangu nikiwa mdogo na daima amekuwa ndiye shujaa wangu. Kwa mtazamo wangu yeye ni bora".

Benzema pia amekuwa akifananishwa na Mfaransa mwenzake Zinedine Zidane. "Ni kutia chumvi kunifananisha mimi na yeye, lakini ni yeye ni 'role model' wangu katika kile ninachofanya na ninachotaka kufikia. Huwa namuomba ushauri na huwa ananipatia. Natumai kuwa na maisha tofauti na yake ya soka, lakini natumai nitakuwa na mafanikio kama yake".

No comments:

Post a Comment