Saturday, October 27, 2012

ARSENAL WAELEKEA KUCHOSHWA NA ARSENE WENGER... TAARIFA ZAVUJA LEO ZIKIDAI KWAMBA WAMEANZA KUMFUKUZIA PEP GUARDIOLA... ABRAMOVICH NAYE AMTAKA GUARDIOLA AIPE MATAJI CHELSEA KAMA BARCA...!

Guardiola akionyesha tuzo yake ya Kocha Bora wa Mwaka wa Dunia 2011.
Guardiola na binti yake wakikatiza mitaa ya jiji la New York, Marekani mwezi uliopita.
Guardiola na familia yake wakikatiza mitaa ya jiji la New York, Marekani mwezi uliopita.
LONDON, England
Kambi ya Pep Guardiola imekuwa katika mazungumzo na Arsenal huku Chelsea pia ikimfukuzia kocha huyo anayetajwa kuwa mbioni kutua jijini London.

Guardiola ambaye ni kocha wa zamani wa Barcelona anataka kufundisha katika klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya England, hasa yenye maskani yake jijini London.

Gazeti la Telegraph limesema leo kuwa mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich amekuwa shabiki wa Guardiola kwa muda mrefu na kwamba sasa anaangalia uwezekano wa kumpa madaraka ya kuifundisha klabu yake yake baada ya kuondoka kwa kina Carlo Ancelotti nan Andre Villas Boas.

Wawakilishi wa Guardiola, kupitia watu wa kati, pia wamwasiliana na Arsenal kuhusiana na uwezekano wa kuwa na nafasi wazi ya kocha hapo baadaye. Lakini, licha ya kuanza vibaya kwa Arsenal na kuwapo mwanzo mzuri wa Chelsea, kocha Arsène Wenger anaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kubaki na kibarua chake kulinganisha na Di Matteo (kocha wa Chelsea).

“Pep anataka kufundisha jijini London na anaangalia klabu yenye mipango sahihi,” kilisema chanzo kimoja kilicho karibu na Guardiola.

No comments:

Post a Comment