Tuesday, September 25, 2012

ZLATAN IBRAHIMOVIC ATABIRIWA KUIFUNGIA PSG MABAO ZAIDI YA 30 MSIMU HUU

Zlatan Ibrahimovic
PARIS, Ufaransa
ZLATAN Ibrahimovic atakuwa mchezaji wa kwanza baada ya Jean-Pierre Papin kufunga magoli yanayofika 30 katika msimu mmoja wa Ligue 1, Ligi Kuu ya Ufaransa, Papin ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa ametabiri leo.

Msweden Ibrahimovic, aliyejiunga na Paris St Germain akitokea AC Milan wakati wa kuelekea mwisho wa dirisha la usajili uliopita wa majira ya kiangazi, tayari ameshafungha magoli saba katika mechi sita za mwanzo wa msimu na anaelekea kuvunja rekodi ya magoli 30 iliyowekwa na Papin mwaka 1990.

"Anatisha. Nafikiri atvunja rekodi yangu ya mabao 30 katika msimu mmoja," Papin, aliyefunga mabao hayo wakati akiichezea Olympique Marseille, ameiambia Le Parisien.

No comments:

Post a Comment