Tuesday, September 25, 2012

WAYNE ROONEY APONA... SASA YUKO FITI KUIVAA TOTTENHAM JUMAMOSI

Wayne Rooney
LONDON, England
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney, ambaye hajacheza mwezi mzima baada ya kuumia vibaya paja dhidi ya Fulham huenda akarudi uwanjani wiki hii na kuungana kikosini na wachezaji wenzake wa Manchester United.

Mguu wa Rooney uliumizwa vibaya baada ya mshambuliaji huyo kugongana na mshambuliaji wa Fulham,  Hugo Rodallega kwenye Uwanja wa Old Trafford Agosti 25, lakini sasa anaweza kucheza dhidi ya Newcastle United katika mechi yao ya Kombe la Carling au dhidi ya Tottenham Hotspur katika mechi ya Ligi Kuu ya England Jumamosi.

"Hayuko mbali sana," kocha Alex Ferguson amewaambia waandishi wa habari.
"Amekuwa akifanya mazoezi makali na pia kujituma sana."

No comments:

Post a Comment