Thursday, September 27, 2012

WENGER AKIRI THEO WALCOTT ANATISHA MBAYA AKICHEZA KAMA STRAIKA WA KATI... NI BAADA YA NYOTA HUYO KUIONGOZA ARSENAL KUIUA COVENTRY 6-1

Theo Walcott
LONDON, England
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amegusia kwamba Theo Walcott anaweza kutimiziwa matakwa yake ya kucheza kama straika wa kati baada ya kutupia mabao mawili yaliyoisaidia klabu hiyo kuibuka na ushindi mnono wa 6-1 dhidi ya Coventry City katika mechi yao kuwania Kombe la Capital One (zamani Kombe la Carling) jana.

Mchezaji huyo mwenye miaka 23 yuko katika mgogoro wa muda mrefu kuhusiana na kusaini mkataba mpya wa kumbakiza Arsenal, akieleza dhamira yake ya kutaka achezeshwe katika nafasi ya kushambulia kutokea katikati ya uwanja badala ya kuwa winga kama sharti lake la kuendelea kuichezea timu ya kocha Wenger.

Na Mfaransa Wenger amefichua kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa England ameitumia vyema nafasi ya kucheza kati aliyopewa jana kwa kufunga mabao ya kusisimua.

"(Walcott) sasa ni mmaliziaji mzuri. Anatisha sana awapo mbele ya goli," Wenger aliwaambia waandishi wa habari.

"Hivi sasa kuna ushindani mkali (nafasi ya ushambuliaji wa kati) na timu inafanya vizuri. Nafasi yake itakuja tu. Hivi sasa tunapaswa kuwa wavumilivu.

"Sipingi (Walcott kucheza kati) kabisa."

Wenger pia alielezea furaha yake kuona kwamba Olivier Giroud akifunga golio lake la kwanza tangu alipotua klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Montpellier.

Kocha huyo mwenye miaka 62 alimwagia sifa pia kiungo mchezeshaji Andrey Arshavin, aliyeanza kikosini kwa mara ya kwanza tangu Januari.

"Nafasi yake bora zaidi sasa ni kucheza nyuma ya straika. Hapo ndipo uwezo wake na mbinu kali za kusoma mchezo zinapozaa matunda," Wenger alitania.

"Anapocheza pembeni wakati mwingine huwa na wakati mgumu kwani hulazimika kupanda na kushuka. Wakati anapocheza kati, anakuwa mkali zaidi.

No comments:

Post a Comment