Thursday, September 27, 2012

JACK WILSHERE WA ARSENAL SASA 'FITI' KUCHEZA ... NAHODHA THOMAS VERMAELEN NAYE APONA

Jack Wilshere

Jack Wilshere akijifua mazoezini
Thomas Vermaelen
LONDON, England
Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere atacheza mechi yake ya kwanza tangu Julai 2011 wakati atakapoichezea timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 21 wa klabu yake Jumatatu
.

Wilshere alikuwamo katika kikosi cha kwanza cha mabingwa mara 13 wa England kabla hajaumia kifundo cha mguu ambacho baadaye kilimsababishia jeraha baya la goti.

"Ni habari njema kwake kurudi uwanjani," kocha Arsene Wenger aliuambia mkutano na waandishi wa habari leo kuelekea mechi yao ya Jumamosi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya vinara Chelsea.

"Wakati unapokuwa nje kwa muda mrefu sana, ni jambo kubwa kurejea. Ni tukio la kusismua sana kwake," aliongeza Mfaransa Wenger.

"Kipindi alichopita kitamfanya awe ngangari zaidi. Ni kipimo kizuri cha uimara wa kifikra."

Wilshere alionyesha kiwango cha juu na kupenya katika kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya England kabla hajaumia katika mechi za kirafiki za maandalizi ya msimu mwaka jana na baadaye akakumbana na changamoto kadhaa wakati akijiuguza, ingawa Wenger hajawahi kuhofia juu ya kurejea uwanjani kwa yosso huyo.

"Siku zote nimekuwa nikiamini kwamba atarejea. Wilshere amekuwa akipanda na kushuka. Alikuwa na malengo, hasa katika miezi mitatu iliyopita," Wenger alisema kumzungumzia kiungo huyo mwenye miaka 20, ambaye aliungana na wenzake kushiriki mazoezi kamiliwiki iliyopita.

"Kidogo tunapaswa kuwa wanagalifu. Tunapaswa kumuongoza vizuri. Anahitaji mechi chache za kuanzia katika kikosi cha wachezaji wa akiba," ameongeza Wenger.

Wakati huohuo, kulikuwa na habari nzuri zaidi kwa Arsenal wakati Wenger aliposema kwamba beki Thomas Vermaelen atakuwa 'fiti' pia kwa mechi ya keshokutwa Jumamosi dhidi ya Chelsea ambao ni mabingwa wa Ulaya itakayoanza saa 8:45 (kwa saa za Kibongo).

No comments:

Post a Comment