Thursday, September 27, 2012

FALCAO: SINA MPANGO WA KUSHINDANA KUFUNGA MABAO NA CRISTIANO RONALDO NA LIONEL MESSI

Radamel Falcao
MADRID, Hispania
STRAIKA wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao aliripotiwa mwanzoni mwa msimu huu kwamba yuko tayari kushindana katika kuwania tuzo ya Mfungaji Bora wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania (pichichi) dhidi ya wanasoka wakali zaidi duniani kwa sasa, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Hata hivyo, leo Falcao amekana na kuweka wazi kwamba dhamira yake kuu ni kuisaidia Atletico Itwae mataji na sio kushindana na wawili hao.

"Sijawahi kusema kwamba ninataka kushinda na Cristiano Ronaldo na Messi," Falcao alikaririwa akisema katika gazeti la AS.

"Ninachokitaka ni kufunga mabao tu ya kuisaidia timu yangu, si kitu kingine. Mwishowe tutaona nimefikia wapi.

"Kitu muhimu zaidi ni kuona timu inatimiza malengo yake. Tunashinda na timu nyingine 19, na wala sio dhidi ya Real Madrid na Barcelona tu."

Falcao ameshafunga mabao saba hadi sasa baada ya mechi tano za La Liga msimu huu.

No comments:

Post a Comment