Sunday, September 30, 2012

WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDRICK SUMAYE AGARAGAZWA VIBAYA NA DK. MARY NAGU ... NI KATIKA UCHAGUZI WA KUWANIA UJUMBE WA NEC (CCM) WILAYA YA HANANG

Haa haa haaaa...! Dk. Mary Nagu
Pole Mzee...! Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye

Waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, amegaragazwa vibaya katika kinyang'anyiro cha kuwania ujumbe wa NEC wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Wilaya ya Hanang mkoani Manyara baada ya kushindwa mbele ya Dk. Mary Nagu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hanang.

Katika uchaguzi huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na kufanyika katika eneo la Katesh, Dk. Nagu aling'ara na kumfunika vibaya waziri mkuu huyo wa enzi za utawala wa serikali ya awamu ya tatu ya Rais Benjamin Mkapa baada ya kuzoa kura 648 dhidi ya 481 kati ya kura 1,170 zilizopigwa.

Sumaye pia alikubali kushindwa katika uchaguzi huo na Dk. Nagu ambaye pia ni Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji, alisema amefurahi kwavile matokeo hayo yamedhihirisha kuwa wanawake pia wanaweza.


Kabla ya kufanyijka kwake, uchaguzi huo ulikuwa gumzo kutokana na upinzani mkali uliokuwapo.

No comments:

Post a Comment