Sunday, September 30, 2012

NYILAWILA AELEZA KISA CHA KUDUNDWA VIBAYA KWA K.O NA FRANCIS CHEKA.... ADAI ET, JAMAA ANA FAULO KIBAO ZA KISIRISIRI... CHEKA ASEMA AMEFURAHI KWA VILE AMEMZIBA MDOMO NYILAWILA ALIYEKUWA AKICHONGA CHONGA SAAAAANA.....!

Bondia Kalama Nyilawila aliyedundwa vibaya jana kwa K.O ya raundi ya sita na Francis Cheka amesema kuwa mpinzani wake si lolote, bali kilichomsaidia hadi akashinda ni ujanja wake wa klucheza faulo nyingi za kisirisiri.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa pambano lao la kusisimua lililofanyika jana kwenye ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na maelfu ya watu, Nyilawila alisema kuwa yeye hakushindwa kwa sababu ya kuishiwa pumzi kama watu wengi wanavyodhani, bali ni kwa sababu tu ya "ujanja-ujanja" wa mpinzani wake ambaye alikuwa akimfanyia faulop lakini refa hakuwa akiziona na wala watazamaji.


"Cheka amenishinda sio kwa sababu ya pumzi... ila anacheza faulo za kiujanja sana," amesema Nyilawila ambaye kabla ya jana, alishapigwa kwa pointi na Cheka lakini akawa hakukubali kushibndwa na badala yake kudai kuwa majaji walimbeba mpinzani wake.


Kwa upande wake, Cheka alisema baada ya mechi hiyo kuwa amefurahi sana kwa sababu ushindi wake wa K.O umemzima kabisa mpinzani wake aliyekuwa "akichonga" sana kabla ya pambano hilo na kudai kwamba ni lazima atashinda.

"Nashukuru kuwa nimeweza kushinda kwa sababu Kalama (Nyilawila) alikuwa anaongea sana... sasa naamini wale wote waliokuwa wakiongeaongea watanyamaza," alisema Cheka, ambaye pia aliiomba serikali na makampuni binafsi kujitokeza katika kudhamini mchezo wa ngumi.

Kutokana na ushindi wa kishindo alioupata jana, Cheka sasa anaelekea kukosa mpinzani nchini kwani ameshawatandika zaidi ya mara moja mabondia wote waliokuwa wakiaminika kuwa ni wakali nchini, wakiwamo Rashid Matumla na ndugu yake Hassan Matumla, Mada Maugo na Japhet Kaseba.

No comments:

Post a Comment