Tuesday, September 25, 2012

DEMBA BA: HIVI SASA NINATISHA KULIKO MSIMU ULIOPITA

Straika Demba Ba wa Newcastle akipiga shuti kufunga goli katika mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park,  Septemba 17, 2012.
LONDON, England
STRAIKA Demba Ba amepeleka ujumbe kwa wapinzani wa timu yake ya Newcastle United katika Ligi Kuu ya England kwa kuwaonya akisema: "Hivi sasa nimekuwa mkali zaidi kuliko msimu uliopita."

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal alikuwa gumzo klabuni kwake katika nusu ya kwanza ya msimu wa 2011-12, kabla kiwango chake hakijashuka baada ya kurejea kutoka katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2012).

Hata hivyo, straika huyo wa zamani wa West Ham amekuwa ni miongoni mwa wafungaji wa kutumainiwa zaidi na Newcastle katika mechi za mwanzo wa msimu huu, na Ba anaamini kwamba hivi sasa amekuwa mkali zaidi kulinganisha na miezi 12 iliyopita.

"Sasa najisikia vizuri, nimekuwa nikicheza vizuri na nitaendelea kufanya vizuri kadri nitakavyoweza," Ba ameiambia tovuti rasmi ya Newcastle leo.

"Nadhani hivi sasa niko vizuri zaidi kuliko msimu uliopita," amesema Demba Ba.

No comments:

Post a Comment