Sunday, September 23, 2012

VILANOVA: HAKUNA BIFU LOLOTE KATI YA MESSI NA DAVID VILLA


BARCELONA, Hispania

Kocha wa Barcelona, Tito Vilanova amekanusha taarifa kwamba kuna bifu kali kati ya David Villa na Lionel Messi.

Wawili hao walionekana wakibwatukiana wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania waliyoshinda 2-0 dhidi ya Granada jana.

"Hakuna kitu chochote (kilichotokana na kubwatukiana kati ya Villa na Messi)," Vilanova amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mechi.

"Yeyote aliyewahi kucheza soka anajua kwamba kujibishana ni kitu cha kawaida, na pia ni sehemu ya mchezo.

"Matukio kama yale ni dalili kwamba timu iko hai. Kutoambiana kitu kwa manufaa ya timu kunamaanisha kwamba kuna tatizo kubwa".

No comments:

Post a Comment