Sunday, September 23, 2012

MOURINHO AMWAMBIA SERGIO RAMOS ASIPOKAZA MSULI ATAOZEA BENCHI


MADRID, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho amemtaka Sergio Ramos aongeze jitihada uwanjani ili kurejea katika kikosi cha kwanza.

Ramos aliachwa benchi katika ushindi wa mabao 3-2 walioupata dhidi ya Manchester City katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Mourinho said: "Wachezaji hawajui na kama hawajui, siwezi kuwaambia waandishi wa habari. Hakucheza mechi iliyopita na wote, Pepe na Varane walicheza vizuri sana; haraka, kwa uhakika na malengo. Hakuna yeyote kati yao aliyehusika na mabao mawili tuliyofungwa."

No comments:

Post a Comment