Sunday, September 16, 2012

VICTOR MOSES: NDOTO YANGU KUCHEZEA BARCELONA

Victor Moses wa Chelsea (kushoto) akibanwa na Jose Bosingwa wa QPR wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Loftus Road mjini London, England jana Septemba 15, 2012. Timu hizo zilitoka sare ya 0-0.

KIUNGO mpya wa Chelsea, Victor Moses amebainisha ndoto zake za kuja kuchezea Barcelona siku moja.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 21, aliyehamia Uingereza akitokea Nigeria akiwa na umri wa miaka 11, hivi karibuni alihamia Chelsea akitokea Wigan Athletic kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 9 na akiwa ndio kwanza amecheza mechi moja tu katika klabu yake mpya anawaza kuchezea Barcelona.

"Ilikuwa ni safari ndefu [kutoka Nigeria] na na nataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa ajili yangu mwenyewe, iwe katika soka ama sio soka," Moses alikaririwa katika gazeti la The Guardian.

"Ni lazima nimshukuru Mungu kwa kuwa hapa nilipo, ni kama ndoto iliyokuwa kweli na, kama nitaendelea kufanya kazi kwa bidii, nani anajua, naweza kutua Barcelona siku moja."

No comments:

Post a Comment