Sunday, September 16, 2012

FALCAO NI BORA DUNIANI

Falcao wa Atletico Madrid
Straika wa Colombia, Radamel Falcao akishangia goli alilofunga pamoja na wachezaji wenzake wakati wa mechi yao ya kuwani kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Chile mjini Santiago, Septemba 11, 2012. Picha: REUTERS


KIPA wa Rayo Vallecano, Dani Gimenez amesema nyota wa Atletico Madrid, Radamel Falcao ndiye mshambuliaji bora duniani.

Falcao alifunga 'hat-trick' mbili mfululizo dhidi ya Athletic Bilbao na Chelsea mara moja kabla ya kwenda kuichezea timu yake ya taifa ya Colombia ambapo pia aliifungia katika mechi zote mbili za kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay na Chile.

Gimenez alisema kuelekea mechi yao ya leo usiku: "Falcao ni mmoja wa washambuliaji bora duniani, yuko katika kiwango bora na nafasi kubwa ya Atletico kufanya vizuri inamtegemea yeye, licha ya kwamba wao ni timu nzuri yenye wachezaji wakali.

"Falcao ni mchezaji wa staili nyingine, mshambuliaji halisi wa kati, na mfungaji.

"Ni kweli kila mtu anawazungumzia (Lionel) Messi au Cristiano Ronaldo. Falcao hayuko katika matawi yale kwa sababu anafanya mambo pungufu, lakini katika anachofanya yeye ni bora."

No comments:

Post a Comment