Sunday, September 16, 2012

SIKUTEGEMEA KAMA PARK JI SUNG PIA ASINGEMPA MKONO JOHN TERRY

Anton Ferdinand wa Queens Park Rangers akimpita John Terry wa Chelsea bila ya kumpa mkono wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Loftus Road mjini London jana Septemba 15, 2012.

KOCHA wa QPR, Mark Hughes amesema hakujua kama nahodha Park Ji-sung angeungana na Anton Ferdinand katika kukataa kumpa mkono nahodha wa Chelsea, John Terry kabla ya mechi yao iliyoisha kwa sare ya 0-0.

Ferdinand hakuwapa mikono Terry na Ashley Cole kama ilivyotarajiwa wakati wa kusalimiana kabla ya kuanza kwa mechi baina yao kwenye Uwanja wa Loftus Road jana.

Haikujulikana ni wachezaji wangapi wenzake wa QPR wangeungana naye lakini bado ilikuwa ni mshangao kumuona nahodha Park akifanya hivyo, jambo ambalo lilirudia hata wakati wa kurusha shilingi.

Park alitumia miaka saba akicheza pamoja na kaka yake Ferdinand, Rio, klabuni Manchester United na inawezekana kwamba maamuzi hayo yalitokana na kuonyesha sapoti yake kwa mchezaji mwenzake wa zamani.

Hughes alisema: "Walikuwa na mazungumzo na nilifahamuishwa kwamba baadhi yao wanajiandaa kutowapa mikono na wengine wangewapa.

"Sikujua ni nani wangetoa mikono na akina nani wasingetoa.

"Yalikuwa ni maamuzi binafsi kwa kila mmoja wao."

No comments:

Post a Comment