Tuesday, September 25, 2012

VALENCIA ALIJIANGUSHA - GLEN JOHNSON

Valencia (katikati) akianza kuanguka katika tukio alilodai kuchezewa faulo na Glen Johnson (kulia) huku kipa Pepe Reina akijaribu kuzuia wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool Septemba 23, 2012 

Tukio ambalo Liverpool wanahoji kama lingetokea kwa Suarez angepewa penalti?
Liverpool wanahoji: Ni nani aliyerukia mpira kwa miguu miwili?

BEKI wa kulia wa Liverpool, Glen Johnson amemuita winga wa Manchester United, Antonio Valencia "MDANGANYIFU" kwa penalti aliyopata katika mechi baina yao Jumapili.

Beki huyo wa kulia wa timu ya taifa ya England alikasirika kwani amedai hakumgusa winga huyo wa Ecuado, ambaye amemtuhumu kufanya udanganyifu.

"Nimeangalia video ya tukio lile mara 50 - ingawa sikuhitaji kufanya hivyo - kwa sababu ile haikuwa penalti, sikumgusa, niligongana na Pepe (Reina)," alisema mchezaji huyo wa kimataifa wa England.

"Sifa za mtu huwa zinawaingia watu wakati mwingine na kwa sababu Valencia si mtu wa kujiangusha ndio maana akapewa penalti ile.

"Nakuhakikishia kama jambo kama lile lingemtokea Luis (Suarez) na sio Valencia isingekuwa penalti.

"Lakini mwisho wa yote ule ni udanganyifu, ndivyo watu wanavyouita.

"Huwezi kuelezea (hisia) lakini hutarajii watu wafanye mambo kama yale kwa sasabu wana uwezo mkubwa kuliko vile.

"Hii ni ligi bora duniani lakini unakuta mtu anajiangusha.

"Najua ni ngumu kwa refa wakati tunapikuwa tunakimbia kwa kasi sana lakini katikamechi kubwa wao ndio wanaoleta tofauti na tunatarajia marefa wafanye maamuzi sahihi.

"Tunafanya kazi kwa bidii ili kushinda mechi lakini mnanyang'anywa kirahisi namna ile .... siwezi kuelezea.

"Refa aliniambia kwamba alilazimika kutoa penalti kwa sababu alidhani kwamba nilimgusa. Inafadhaisha kwa sababu sikumgusa."

No comments:

Post a Comment