Tuesday, September 25, 2012

SUAREZ HATA PENALTI HALALI HAPEWI - GERRARD

Tukio ambalo Liverpool wanalilalamikia kwamba Suarez aliangushwa

Suarez akianguka na refa kuamua kwamba alijirusha

WACHEZAJI wa Liverpool, Steven Gerrard na Glen Johnson wamemtetea mchezaji mwenzao Luis Suarez.

Madai ya penalti ya Suarez yalitoswa wakati wa mechi yao ya kipigo cha 2-1 kutoka kwa Manchester United Jumapili.

"Nadhani hata pale Luis anapopata penalti halali sasa hapewi," alisema Gerrard.

"Ni suala la marefa kutomhukumu na kutoa maamuzi yaliyosahihi - kama so penalti wasitoe lakini kama iko wazi watoe.

"Alipewa kadi ya njano dhidi ya Sunderland lakini dhidi ya United ilikuwa ni penalti."

Johnson aliungana na nahodha wake kwa kuongeza: "Kila mmoja anapaswa kufanya kazi yake: wanapaswa kusahau kile wanachokitafuta na kutoa maamuzi na sio kuruhusu mambo ya zamani yaathiri maamuzi yao.

"Wanapaswa kutoa maamuzi sahihi bila ya kuangalia yanamhusu nani."

No comments:

Post a Comment