Monday, September 24, 2012

MISHAHARA MINONO YA WAGENI YAKERA WAZAWA URUSI

Hulk
MOSCOW, Urusi
Nahodha wa timu ya taifa ya Urusi, Igor Denisov amedai kusikitishwa na sera za klabu ya Zenit St Petersburg zinazopendelea wachezaji wa kigeni kwa kuwalipa mishahara minono kulinganisha na wazawa.


"Kwanini wageni walipwe mara tatu ya wachezaji bora zaidi kikosini? Ndiyo maana na mimi nikaomba niongezewe mshahara. Lakini badala yake nikapigwa panga na kocha," Denisov alisema.


"Kama Hulk na Witsel wangekuwa na viwango sawa na Messi na Ronaldo ingekuwa sawa, lakini hawana viwango hivyo. Sasa kwanini kuwe na upendeleo huu kwao katika mishahara?

No comments:

Post a Comment