Thursday, September 13, 2012

JE, UNATAKA KUJIUNGA NA FREEMANSONS? ALIYEKUWA KIGOGO WA CHAMA HILO KUANIKA KILA KITU LEO KUANZIA SAA 3:00 USIKU... NI KATIKA MAHOJIANO YAKE NA MTANGAZAJI GERARD HANDO WA CLOUDS TV

Sir Andy Chande (kushoto) akiwa na Rais Kikwete
Sir Andy Chande (kulia) akiteta jambo na Benjamin William Mkapa mwaka 1989. Hapa ni miaka sita kabla Mkapa hajawa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sir Andy Chande (kulia) akiwa na rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mkapa.
Sir Andy Chande (kulia) akiteta jambo na rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.
Sir Andy Chande (kushoto) akiwa na rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.
Sir Andy Chande (kulia) akiwa na rais mstaafu wa Zanzibar, Amaan Abeid Karume.
Jengo la Freemasons lililopo Posta jijini Dar es Salaam.
Sir Andy Chande (wa tatu kulia) akiwa na viongozi mbalimbali maarufu, wakiwamo mawaziri wakuu wastaafu nchini, Joseph Warioba(kushoto) na Salim Ahmed Salim (kulia).
Sir Andy Chande (kushoto) akiwa na mtangazaji wa Clouds FM, Gerrard Hando.
Aliyewahi kuwa kinara wa kundi la Freemasons katika eneo la Afrika Mashariki, Jayantilal Keshavji Chande maarufu kama Sir Andy Chande, leo  kuanzia saa 3:00 usiku ataanika mambo mengi kuhusiana na undani wa kundi hilo wakati atakapozungumza na mtangazaji Gerrard Hando wa kituo cha televisheni cha Clouds "The Peoples Station".

Akizungumza kupitia kipindi cha Power Breakfast cha redio ya Clouds FM leo asubuhi, mtangazaji Hando ambaye ndiye aliyefanya mahojiano na Sir Chande, amesema kuwa mambo mengi kuhusu undani wa Freemasons na namna wanavyofanya kazi zao, yameelezewa kwa kina na kigogo huyo wa zamani wa kundi hilo duniani.

Amesema kuwa mahojiano hayo yatarushwa kuanzia leo kupitia kipindi chao kipya kiitwacho "The Interview', ambacho kitarushwa kuanzia leo usiku.

Namna ya kujiunga na Freemasons na mahala liliko hekalu la kundi hilo jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kuanikwa na Sir Chande.

Kigogo huyo wa zamani Freemasons amekuwa karibu sana na viongozi wa juu serikalini, wakiwamo marais wastaafu wote wa Tanzania ambao ni hayati baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na hata sasa, anaonekana kuiva vyema na Rais Jakaya Kikwete.

No comments:

Post a Comment