Wednesday, September 12, 2012

SERGIO AGUERO: MAN CITY SASA TUKO 'FITI' KUWACHAKAZA REAL MADRID, BARCELONA

Sergio Aguero wa Manchester City akiugulia maumivu baada ya kupata majeraha wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Southampton kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester, England Agosti 19, 2012.

MANCHESTER, England
Sergio Aguero amesisitiza kwamba Manchester City ya sasa imekamilika na kwamba inaweza 'kuichakaza' Real Madrid wakati timu hizo zitakapokutana katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu Jumanne usiku.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wanajiandaa kushiriki kwa mara ya pili tu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, na waliondolewa mapema kwenye michuano hiyo msimu uliopita wakati wakiwa katika hatua ya makundi, kama walivyokuwa mahasimu wao wa jadi, Manchester United.

Hata hivyo, straika huyo wa kimataifa wa Argentina - mwenye uzoefu wa kucheza dhidi ya Real Madrid wakati alipokuwa kwa mahasimu wao Atletico Madrid, anaamini kwamba klabu yake sasa ni moto wa kuotea mbali na inaweza kupambana vyema timu kali barani Ulaya kama Real na Barcelona katika kuwanuia taji la Ulaya.

“Sijawahi kuwamo katika timu iliyoshinda dhidi yao (Real Madrid) kwahiyo naamini kwamba nikiwa na Man City tutawachapa," Aguero ameiambia Daily Express.

“Itakuwa ngumu. Hivi sasa Real na Barca ni miongoni mwa timu kali duniani, lakini na sisi tuna timu kali pia.”

No comments:

Post a Comment